Training

 

Mpango wa Udhibiti Usio na Udhibiti wa Global

 

Pamoja na shirika linaloshirikiana nalo la CRDF Global, CCSI sasa inaanza mafunzo ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa vya kupinga usambazaji wa silaha kwa lugha kadhaa kote ulimwenguni.

Matukio ya lugha mbili yanayojumuisha ukalimani yameratibiwa kufanyika huko Maputo (Msumbiji), Mombasa (Kenya), Abidjan (Kodivaa), Manila (Ufilipino), Bali (Indonesia), na Jiji la Ho Chi Minh (Vietinamu).

Warsha za siku 2 zinategemea toleo la CCSI la hivi karibuni lililosahihishwa la.

 

Mwongozo wa Utekelezaji wa Vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyowekewa Korea Kaskazini

Mwongozo huo una kurasa 130, zenye ramani, maonyesho na majedwali, ili kujumuisha vipengele vyote ambavyo watendaji wanaviona kuwa ni muhimu, kwenye sura zifuatazo:

 

I. Ufalme pweke wa kudumu

II. Diplomasia ya kijeshi ya Korea Kaskazini na vikwazo vya Umoja wa Mataifa

III. Mashirikisho ya Korea Kaskazini

IV. Mazingira ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa

V. Hatua za vikwazo vya Umoja wa Mataifa

VI. Mfumo wa kutekeleza vikwazo wa serikali-nzima

VII. Mfumo wa kutii vikwazo wa shirika-zima

Read more

Vijitabu hivi viliandikwa kwa ushirikiano baina ya Enrico Carisch na Loraine Rickard-Martin, pamoja na usaidizi wa kitafiti kutoka kwa Ola al-Tamimi, Anastasia Borosova, Won Jang, Jake Sprang, Alfredo Villavicencio na Samantha Taylor.

Kwa ziada, uchunguzi 10 ufuatao wa kifani, uliotayarishwa na washiriki na wataalamu wa mada husika wa CCSI unafanywa upatikane kwa kufasiriwa:

 

Mbinu Dijitali za Kuenda Kinyume na Vikwazo vya Umoja wa Mataifa

Uchunguzi wa Kifani wa Kikosi cha Mtandaoni cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kor ea

 

Imetayarishwa na Ashley Taylor

Sekta ya mtandaoni ni safu mpya ya kutekeleza na kuenda kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Kwa sababu Intaneti inatoa nafasi pepe ya mawasiliano na miamala ya papo ha po, inatoa fursa zisizodhibitiwa na rahisi zaidi kwa wahusika wahalifu wanaokiuka mienend o inayokubalika kimataifa. Matumizi haramu ya teknolojia dijitali ni yanashinda nguvu maen deleo yanayofanywa na wanateknolojia halali, ambao kwa jumla huwa hawaupi kipaumbele usalama wa kimataifa kwenye biashara yao. Read more

Mtekelezaji, mjasiriamali na mtafiti, Ashley Taylor amejitumbuk iza mzima kwenye mwingiliano wa teknolojia dijitali na usalam a wa kimataifa. Kwa kuwa mwanachama wa kizazi cha kwanza cha wajasiriamali wa blokicheni, Taylor ameng'amua mapema madhara yanayoweza kutokana na mawasiliano yanayosimbw a na teknolojia za leja zinazosambazwa kwenye uadilifu wa bia shara na maendeleo ya kijamii. Kwa kufanya kazi na mashirika ya teknolojia na fedha, sasa anashughulika kuunda mpangilio wa kibinadamu unaohusisha teknolojia mpya na vigezo vya ute kelezaji vinavyounga mkono udumishaji wa amani na usalama kimataifa.

 

Kupinga Ufadhili wa Usambazaji

Mafunzo Yaliyong'amuliwa kwenye Mfano wa Usafirishaji wa Chinpo

 

Imetayarishwa na Beatrice Müller

Beatrice Müller ana shahada ya kwanza kwenye Sayansi ya Kisiasa na sh ahada ya uzamili kwenye mafunzo ya Mashariki ya Kati kutoka Chuo Kik uu cha Geneva. Kwa sasa anafanya kazi kwenye nyanja ya udhibiti wa si laha, upingaji usambazaji na upokonyaji silaha, huku pia alipokuwa anaf anya kazi kama mhariri mwenza wa masuala ya mambo ya nje kwenye kituo cha utafiti cha Uswizi kiitwacho foraus. Hapo awali, Bi. Müller alik uwa mkufunzi na kufanya kazi kwenye NGO ya haki za binadamu na Mu ungano wa Mabunge. Read more

Beatrice Müller ana shahada ya kwanza kwenye Sayansi ya Kisiasa na sh ahada ya uzamili kwenye mafunzo ya Mashariki ya Kati kutoka Chuo Kik uu cha Geneva. Kwa sasa anafanya kazi kwenye nyanja ya udhibiti wa si laha, upingaji usambazaji na upokonyaji silaha, huku pia alipokuwa anaf anya kazi kama mhariri mwenza wa masuala ya mambo ya nje kwenye kituo cha utafiti cha Uswizi kiitwacho foraus. Hapo awali, Bi. Müller alik uwa mkufunzi na kufanya kazi kwenye NGO ya haki za binadamu na Mu ungano wa Mabunge.

 

Mashirikisho ya Korea Kaskazini

Uhusiano Wake na Silaha, na Shughuli za Kuvunja Vikwazo

 

Imetayarishwa na Kathrin Kranz

Mashirikisho ni mashirika makubwa yanayoundwa kwa kuunganisha biashara anuwai zilizo kando. Mashirikisho ya Korea Kaskazini yamepangwa na kufdhiliwa vizuri, na yana sifa ya utata zaidi kwenye mbinu zao za kukiuka vikwazo. Mashirikisho ni sehemu muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini na pia ni mbinu ya kupata pesa taslimu. Serikali ya Korea Kaskazini imeunda na/au kuunga mkono ukuaji wa mashirikisho kwa lengo wazi la kujenga uhusiano na nchi zingine kupitia uuzaji wa bidhaa za Korea Kaskazini, zikiwemo silaha na bidhaa na mafunzo husika. Kwa upande mwingine, mashirikisho yameisaidia serikali ipate pesa taslimu na vipuri vinavyohitajika kwenye mradi wake wa usamabazaji wa nyuklia. Read more

 

KATAZO LA BIDHAA ZA ANASA

KUELEWA AHADI YAKE NA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO

 

Imetayarishwa na Kathrin Kranz

Ukiukaji wa katazo la usafiri mara kwa mara hutokea kwenye vichwa vya habari, kama vile ilivyotokea mnamo Februari 2019, wakati maafisa wa Uholanzi walipokamata chupa 90,000 za vodka zilizokuwa zinaelekea Korea Kaskazini. Kwa ziada, miradi ya miundombinu ya wananchi mabwenyenye wa Korea Kaskazini yamekamilishwa, kama vile sinema ya 4D na Masikryong Ski Resort, ambayo ina lifti za kuteleza barafuni na magari ya kuteleza barafuni. Ripoti za vyombo vya habari pia zinarejelea “vipodozi na vitamini” kama bidhaa za anasa kwa wananchi wa Korea Kaskazini. Kwa kweli, mnamo 2018, Yoon Sang-Hyun, mtungaji sheria wa Korea Kusini, alidai kuwa Korea Kaskazini ilitumia angalau milioni $640 ili kuingiza nchini bidhaa za anasa kutoka Uchina mnamo 2017. Mifano hii inaweza kutazamwa kwa muktadha wa maswali mapana yanayoibuka kwenye muktadha wa katazo la bidhaa za anasa: ni nini bidhaa za anasa, na nchi tofauti zinafafanua vipi “bidhaa za anasa”? Je, ni mataifa gani yaliyolegea kwenye kutenganisha bidhaa za anasa na bidhaa za kawaida za wateja? Na, muhimu zaidi, sekta binafsi inaweza kuhakikisha kivipi utiifu wa katazo la bidhaa za anasa, ambayo inaweza kuhitaji kuzingati ufasiri na utenda kazi unaobadilika wa mataifa anuwai? Ripoti hii inashughulikia maswali haya, na inatoa mifano inayosaidia kuangazia utata unaohusika ambao unaweza kusaidia kuongoza sekta binafsi ili iweze kulitii katazo. Ripoti pia inasisitiza ubunifu wa katazo la bidhaa za anasa. Kwa kutofafanua maana ya bidhaa za anasa na kuweka wazi kuwa katazo hakijawekewa kikomo kwa bidhaa fulani tu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliunda aina ya vikwazo inayowaudhi mabwenyenye wa Korea Kaskazini bila kuathiri vibaya wananchi wa kawaida wa Korea Kaskazini. Read more

Kathrin Kranz ana Ph.D. ya Mafunzo ya Amani na Sayansi ya Kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha Notre Dame, na LL.M. ya Sheria ya Kimataifa ya Umma kutoka Shule ya Uchumi na Sayansi ya Kisiasa ya London. Utafiti wake unaangazia biashara ya kimataifa ya silaha, vikwazo vya uchumi, na taasisi za kimataifa.

Imetayarishwa na Mark Duncan

Mfumo wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa unaolenga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea ni mfumo mkali zaidi uliopo, unaolazimu serikali zitekeleze mkusanyiko tata wa majukumu ya kutekeleza kisheria na kuripoti;

Mataifa barani Afrika yanaweza kuathirika kwa urahisi na ukwepaji vikwazo kwa ajili ya uhusiano wao wa kibiashara wa muda mrefu na Korea Kaskazini uliokuwepo kabla ya kuidhinishwa kwa mfumo wa vikwazo lakini ambao huenda ukawa si halali kisheria baada ya 2006, unarahisisha ukwepaji unaofanywa na Korea Kaskazini, raia na mashirika yake;

Ili kurahisisha utiifu, mwongozo huu unatoa muhtasari wa aina za hatua za vikwazo zilizowekewa Korea Kaskazini, juhudi za utekelezaji kisheria na majukumu ya kuripoti. Read more

Mark Duncan ni mwanafunzi aliyehitimu na mtafiti mwenye uzoefu mwingi kwenye upokonyaji silaha, kupinga usambazaji, na udhibiti wa silaha. Kwa sasa yeye ni mkufunzi kwenye Ziara ya Kudumu ya Afghanistani kwenye Umoja wa Mataifa. Hapo awali, alikuwa mkufunzi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Upokonyaji Silaha, Baraza la Masuala ya Kimataifa la Urusi na Kituo cha Kimataifa cha Kuchambua Usalama. Alihitimu kutoka UCL na Shule Kuu ya Uchumi, Mosko na Shahada ya Uzamili ya Kimataifa ya Uchumi, Nchi, na Jamii: Amani na Usalama Atajiunga na Ofisi ya Jumuiya ya Madola na Mambo ya Nje kama Mtiririshaji Upesi wa Huduma za Kiraia mbeleni mwaka huu.

Imetayarishwa na Shawna Meister

Ili kufanya juhudi ya kupunguza na mbeleni kukomesha shughuli ambazo si za usambazaji zinazofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK), Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) limeidhinisha vikwazo vinavyolenga watu binafsi na mashirika maalum (walioorodheshwa) wanaoaminiwa kuwa, au wanaofanya aina hizi za ukiukaji huku wakijua wanayoyafanya. Nchi wanachama za Umoja wa Mataifa na mashirika yanayojumuishwa kwenye mamlaka yao (k.v., biashara, mawakala ya serikali, raia, n.k.) yanatarajiwa kutekeleza kisheria vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, maelezo ya kutambua na kufuatilia shughuli za walioorodheshwa mara nyingi huwa ni kidogo au ni taabu kuipata. Ili kusaidia kukuza uwezo wa nchi kutekeleza vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya wakiukaji wa Korea Kaskazini, ni muhimu kujua sifa za pamoja za shughuli na ukiukaji wa kanuni, zinazoshirikiwa na vikundi hivi kama mbinu ya ziada ya kubainisha wakiukaji hawa au wakiukaji wengine wa vikwazo wawezekanao. Uchunguzi huu wa kitafiti unakagua sifa za pamoja za watu binafsi na mashirika yaliyoorodheshwa kwenye mfumo wa Korea Kaskazini, na unatoa mapendekezo yanayoweza kuidhinishwa na mataifa na wahusika wengine husika kuhusiana na wakiukaji hawa na wakiukaji wengine wawezekanao. Read more

Imetayarishwa na Shawna Meister

Watu binafsi na mashirika yanayokiuka vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) pia mara nyingi huwa yanatekeleza ukiukaji madhubuti wa sheria na kanuni za nchi. Shughuli za usambazaji zinazotekelezwa na watu binafsi na mashirika yaliyoorodheshwa ya Jamhuti ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DPRK) zinaweza kuwa na madhara, miongoni mwa mengine, kwa usalama wa nchi wa taifa, uadilifu wa taasisi za fedha za nchi, kanuni za uuzaji nje, au udhibiti wa mipaka. Kwa mfano, usafirishaji wa nyenzo au bidhaa zozote zilizowekewa vikwazo mara nyingi huwa zinhitaji kauli bandia za mamlaka za ushuru, kwa kutoa hati bandia, au kutoa hongo kwa maajenti wa mipaka. Matendo haramu husiani pia yanaweza kuhusishwa na hatari za ziada kwa nchi, kama vile mpito haramu wa nyenzo hatari zinazohatarisha afya na usalama wa yoyote anayeshughulikia usafirishaji huu, au ambazo, kunapotokea ajali, zinaweza kusababisha maafa mengi yaliyosambaa ya binadamu. Ingawa nci zinafanya juhudi ili kujilinda dhidi ya ukiukaji uwezekanao wa sheria zao wenyewe, inaweza kuwa taabu kwa nchi kutambua shughuli husiani zinazofanywa na watu binafsi na mashirika yanayoorodheshwa. Muhtasari huu utasaidia kufafanua ukiukaji haramu au unaovunja kanuni ambao umeonekana au kudokezwa ambao unaweza kuhusishwa na ukiukaji tofauti wa vikwazo. Read more

Shawna Meister - Mchangiaji Mkuu wa CCSI

Mchambuzi wa sera na utafiti, Shawna Meister amefanya kazi na CCSI tangu ilipanzishwa kwenye miradi anuwai kwa miaka minane iliyopita. Historia yake inajumuisha kuchambua kazi ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwenye juhudi za jumla za kusuluhisha vita, vita vya wenyewe kwa wenyewe barani Afrika na kwenye Mashariki ya Kati, changamoto za kutekeleza sheria za vikwazo vya kupinga usambazaji. Hivi karibuni, kama sehemu ya jitihada ya utafiti wa kuainisha ya CCSI, Shawna ameongoza uchambuzi wa sifa na shughuli za watu binafsi na mashirika yaliyoorodheshwa ili kutambua ruwaza na uhusiano ndani ya na kwenye mifumo ya vikwazo. Ameandika machapisho kadhaa yakiwemo kuandika ripoti za kiufundi na kichambuzi, uchunguzi wa kifani, makala ya majarida, na amechangia kwenye miongozo ya kupinga usambazaji na vitavu vyote ambavyo vimechapishwa na CCSI. Uhodari wa Shawna unajumuisha usimamizi wa miradi ya utafiti yenye daraja anuwai na kugeuza uchambuzi na maelezo tata yawe bidhaa zinazoweza kutumika kama vile miongozo ya mafunzo, miongozo ya kielimu, rasilimali na vifaa vya umma, na tovuti.

Imetayarishwa na Thomas Bifwoli

Mnamo Aprili 2019, Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato ya Kenya (KRA) iliripoti kuwa kupitia ushirikiano na Polisi wa Kimataifa (Interpol), iliweza kuyapata tena magari kwenye poti ya Mombasa . Ripoti pia ilisema kuwa bidhaa zizo hizo zitarudishwa Uingereza (Kule zilipotoka). Mnamo Mei, Shirika la Utangazaji la Briteni (BBC) liliripoti ufutaji kazi wa Naibu wa Rais wa Gabon, pamoja na waziri wa misitu, baada ya “kontena 300 za kuni kupotea” kwenye poti nchini Gaboni, iliyoripotiwa kuwa inaelekea nchini Uchina. Walifutwa na rais, Ali Bongo.

Mifano hii miwili ni miongoni mwa hali nyingi za uvukaji mipaka ambazo zinaendelea kuripotiwa na nchi wanachama za Shirika la Ushuru Ulimwenguni (WCO). Kinadharia, kwa usaidizi wa WCO, kupambana na mitandao/mifumo ya uhalifu ya kienyeji na kimataifa ya kuvuka mipaka, kama ile iliyorejelewa hapo juu, hakujawahi kuwa rahisi zaidi. Read more

Imetayarishwa na Thomas Bifwoli

Usimamizi na udhibiti wa mipaka ni mojawapo kati ya changamoto zinazokumba nc hi nyingi. Kwenye ulimwengu wa kimataifa, mamlaka za serikali ni lazima zisawazish e baina ya kudumisha usalama na kurahisisha biashara halali kwa upesi. Pasipokuw epo usawazisho huo, usafirishaji haramu, ulanguzi na uhamiaji haramu, uhalifu wa k imafia, na ugaidi utanawiri.

Inabidi wakala ya kawaida ya kudhibiti mipaka izidi kujibadilisha ili kudumu kwenye ulimwengu usiokuwa na ‘’mipaka". Huu ni ulimwengu unaendeshwa na yafuatay o:

Mipaka wazi: mpaka ni zaidi kuliko mivuko ya kawaida mipakani. Mipak a mipana ya ardhi isiyosimamiwa na watu, miongoni mwa mengine, inasababi sha changamoto za kipekee kwa mawakala ya mipaka. Ni lazima mamlaka hu sika ziendelee kutafuta suluhisho za changamoto hizi.
Usafiri wa watu unaozidi kuongezeka, wa kiharamu na kihalali: inabidi s erikali zibuni njia mpya za kudhibiti mtiririko huu ulioongezeka.
Ongezeko la kiasi cha biashara: kuna haja iliyoongezeka ya kushughulik ia changamoto kama vile usafirishaji wa bidhaa haramu.

Serikali pekee haziwezi kudhibiti wala kutimiza malengo haya. Sawa, kuliko hapo aw ali, kuna haja ya kuhusisha sekta binafsi kwenye kushughulikia changamoto za usim amizi na udhibiti wa mipaka. Kama vile ilivyo hali, Mamlaka za ushuru na mawakala mengine ya mipaka ulimwenguni yanazidi kuhusisha sekta binafsi kwa njia moja au nyingine. Hii inamaanisha kuwa ni lazima mawakala ya kusimamia udhibiti wa mipa ka yafafanue upya kazi yao, yajibadilishe, yawafunze upya wafanyakazi wake, na yaj enge upya uwezo wao wa kiufundi ili uwiane na matakwa haya mapya. Read more

Imetayarishwa na Thomas Bifwoli

Utekelezaji wa Vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unahitaji nia nzuri kutoka kwa nchi wanachama na ufanisi na kuwa tayari kwa taasisi anuwai miongoni mwa Nchi Wanachama za Umoja wa Mataifa.

Mojawapo kati ya taasisi muhimu ni usimamizi wa Mamlaka za Ushuru uliopewa vifaa vinavyohitajika na pia unaoungwa mkono. Mamlaka za Ushuru zinafanya shughuli muhimu kama safu ya kwanza ya ulinzi kuhusiana na kudhibiti yale yanayoingia nchini. Vivyo hivyo, pia ni safu ya mwisho ya ulinzi pale bidhaa zinapotoka nchi fulani. Ili kuweza kufanya hivi kwa ufanisi, sheria zinazohitajika kuunda mpangilio wa kisheria zinahitaji kuundwa. Hii haihusishi tu bidhaa za nchi zilizowekewa Vikwazo vya Umoja wa Mataifa, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DPRK), lakini pia bidhaa zote chini ya udhibiti wa Mamlaka yake ya Ushuru. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imebuni sheria sawia za mamlaka za ushuru ambazo zinadhibiti mtiririko wa bidhaa kuelekea na kutoka nchini, kwa mujibu wa maafikiano ya EAC ya 1999. Tathmini fupi ya sheria hii inadokeza ukosefu wa uwazi kuhusiana na kazi ya Mamlaka za Ushuru kwenye udhibiti wa nyenzo zilizopigwa marufuku kama ilivyoamrishwa kwa nchi zote wanachama kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Read more

Thomas Bifwoli amefanya kazi na Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato Nchini Kenya (KRA); na aliidhinishwa awe Mkubwa wa Ofisi wa Ofisi ya Ushirikiano ya Upelelezi wa Kieneo ya Shirika la Ushuru Ulimwenguni ambayo ni ya Afrika Mashariki na Kusini (WCO RILO ESA). Alifanya kazi kama mratibu wa kundi la wataalamu wa ufuatilizi wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.